Ufafanuzi msingi wa kamata katika Kiswahili

: kamata1kamata2

kamata1

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  shika kwa nguvu kitu kinachokimbia au mtu anayekimbia au kutoroka; tia nguvuni.

  gwia, kota, nasa, bwia, shika

 • 2

  shika vizuri bila ya kuacha; shika sana.

  ‘Kamata usukani wa motokaa’
  koroweza

 • 3

  ‘Kamata koo’
  kaba

Matamshi

kamata

/kamata/

Ufafanuzi msingi wa kamata katika Kiswahili

: kamata1kamata2

kamata2

nominoPlural kamata

 • 1

  aina ya ugonjwa unaomshika mtu ghafla.

Matamshi

kamata

/kamata/