Ufafanuzi msingi wa kofi katika Kiswahili

: kofi1kofi2

kofi1

nomino

 • 1

  pigo la upande wa ndani wa kiganja.

 • 2

  upigwaji wa pamoja wa vitanga viwili vya mikono k.v. wakati wa kufurahikia jambo.

  ‘Wachezaji walipokuwa wakiingia uwanjani watazamaji waliwapigia makofi’

Ufafanuzi msingi wa kofi katika Kiswahili

: kofi1kofi2

kofi2

nomino

 • 1

  ngoma ya pungwa ambayo hupigwa ili kumuita pepo wa mteja.

Matamshi

kofi

/kOfi/