Ufafanuzi wa matamvua katika Kiswahili

matamvua

nominoPlural matamvua

 • 1

  nyuzinyuzi zinazoachwa kama nakshi kwenye pindo la kitambaa k.v. kikoi.

 • 2

  nyuzi ambazo hazikusokotwa bali zimefumuliwa kidogo na kutiwa kasi.

  ‘Nyuzi za matamvua’

 • 3

  nyuzinyuzi kwenye shavu la samaki ambazo huchuja hewa kutoka kwenye maji ili iingie mwilini mwa samaki.

 • 4

  nyuzinyuzi za ufagio wa kupigia deki.

Matamshi

matamvua

/matamvuwa/