Ufafanuzi msingi wa randa katika Kiswahili

: randa1randa2randa3

randa1

nomino

 • 1

  kifaa cha seremala chenye kisu kinachotumiwa kusawazishia mbao.

  ‘Piga randa’

Matamshi

randa

/randa/

Ufafanuzi msingi wa randa katika Kiswahili

: randa1randa2randa3

randa2

kitenzi elekezi

 • 1

  sawazisha ubao kwa kutumia randa.

  ‘Mbao hizi hazikurandwa vizuri’

Asili

Kaj

Matamshi

randa

/randa/

Ufafanuzi msingi wa randa katika Kiswahili

: randa1randa2randa3

randa3 , randaranda

kitenzi sielekezi

 • 1

  pita huku na huku na kujigamba.

  tamba

 • 2

  zunguka huku na huko bila ya kazi au haja maalumu.

  huni, zurura