Ufafanuzi wa samehe katika Kiswahili

samehe

kitenzi elekezi~ea, ~eana, ~eka, ~esha, ~ewa

 • 1

  acha kuwa na kinyongo kwa jambo baya ambalo umetendewa.

  ‘Japo umenitukana lakini nimekusamehe’

 • 2

  acha mtu huru baada ya kutenda kosa fulani.

  feleti

 • 3

  kubali kwa hiari kuacha haki yako k.v. pesa iliyoko kwa mwingine.

  ‘Amemsamehe deni la shilingi mia alizokuwa anamdai’

Asili

Kar

Matamshi

samehe

/samɛhɛ/