Ufafanuzi msingi wa sihi katika Kiswahili

: sihi1sihi2

sihi1

kitenzi elekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa

 • 1

  sema na mtu kwa namna ya kumtaka akubali kutimiza jambo ambalo hataki kulifanya au kulifanya kwa haraka.

  ‘Alikuwa hataki kupatana na ndugu yake lakini nikamsihi mpaka akakubali’
  nasihi, rai, bembeleza, sairi

Matamshi

sihi

/sihi/

Ufafanuzi msingi wa sihi katika Kiswahili

: sihi1sihi2

sihi2

kitenzi elekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa

 • 1

  thibitika kuwa ni sawa au kweli.

  ‘Haisihi mtu kuolewa na kaka yake’
  ‘Imesihi kwamba kitu hiki si chako’

Matamshi

sihi

/sihi/