Ufafanuzi wa sikia katika Kiswahili

sikia

kitenzi elekezi~ka, ~wa

 • 1

  pokea mawimbi ya sauti kwa kutumia sikio.

  pulika

 • 2

  fuata amri.

  ‘Mtoto huyu kila akikanywa hasikii’
  tii

 • 3

  kuwa na hisi fulani.

  ‘Nasikia harufu mbaya’

Matamshi

sikia

/sikija/