Ufafanuzi wa susu katika Kiswahili

susu

nominoPlural susu

 • 1

  nguo inayofungwa k.v. kwenye kitanda, kama pembea na inayotumiwa kulazia watoto wadogo na kuwabembeleza.

 • 2

  mlezi

 • 3

  kitu chenye umbo la kata ya kubebea mtungi, kitengenezwacho kwa kamba au miyaa, kinachoning’inizwa darini na hutumiwa kuwekea sahani au chungu cha chakula ili kukihifadhi dhidi ya k.v. wadudu au paka.

  tundu

Matamshi

susu

/susu/