Ufafanuzi wa uchungu katika Kiswahili

uchungu

nominoPlural uchungu

  • 1

    hisi anazokuwa nazo mtu baada ya kufikwa na jambo la kuumiza k.v. kujikata, kujigonga au jambo la kutia huzuni.

  • 2

    maumivu anayokuwa nayo mwanamke mjamzito anapokaribia kujifungua.

  • 3

    hali anayoihisi mtu kinywani baada ya kuramba au kula kitu kisicho kitamu k.v. shubiri, kwinini, mchunga au pakanga.

Matamshi

uchungu

/utʃungu/