Ufafanuzi msingi wa zua katika Kiswahili

: zua1zua2zua3

zua1

kitenzi elekezi~lia, ~liana, ~lika, ~lisha, ~liwa

 • 1

  tunga au sema maneno yasiyokuwa ya kweli; sema uongo.

  ‘Hayo ameyazua yeye, lakini sivyo mambo yalivyokuwa’
  singizia

Matamshi

zua

/zuwa/

Ufafanuzi msingi wa zua katika Kiswahili

: zua1zua2zua3

zua2

kitenzi elekezi~lia, ~liana, ~lika, ~lisha, ~liwa

 • 1

  anzisha jambo baya ambalo halikuweko katika jamii.

  ‘Ni nani aliyeuzua huu mtindo wa nguo fupi?’

Matamshi

zua

/zuwa/

Ufafanuzi msingi wa zua katika Kiswahili

: zua1zua2zua3

zua3

kitenzi elekezi~lia, ~liana, ~lika, ~lisha, ~liwa

 • 1

  vuta au fukua kitu kilichofukiwa.

  fukua

Matamshi

zua

/zuwa/