Ilani ya kisheria

Ilani hii ya kisheria inahusu haswa tovuti hii ya oxforddictionaries.com ("Tovuti") na tanzu zake na inasimamia utumiaji wako wa Tovuti hii na tanzu zake. Kwa kutumia Tovuti hii, unakubali vitendo vilivyofafanuliwa katika taarifa hii.

Unaweza kufikia sehemu fulani za Tovuti bila kujisajili au bila kutoa maelezo yako kwa Oxford University Press ("OUP", "tu", "sisi" au "-etu").

Kwa vile maelezo yaliyoko kwenye Tovuti huenda yawe ambayo hayajakamilika, yaliyopitwa na wakati au yasiyo sahihi na huenda yawe na makosa ya kiufundi au ya kimaandishi, OUP ina haki ya kusasisha Tovuti hii kwa kuhusisha uamuzi wetu pekee. Kwa hivyo, maelezo ya aina hii yanaweza kubadilishwa au kusasishwa bila ilani.

Tuna haki ya kufanya mabadiliko katika ilani hii ya kisheria. Mabadiliko yoyote tunayoweza kufanya katika ilani hii ya kisheria yatachapishwa kwenye ukurasa huu na, panapofaa, tutakuarifu kupitia barua pepe pia. Masharti fulani ya ilani hii ya kisheria huenda yatawaliwe na masharti na ilani za kisheria zilizoonyeshwa wazi zinazopatikana katika kurasa mahususi za Tovuti.


Majina ya Watumiaji na Nywila

Pale ambapo umejisajili kwenye Tovuti na umepewa jina la mtumiaji pamoja na nywila, unakubali kutopeana jina lako la mtumiaji na/au nywila yako kwa yeyote yule. Ikiwa jina lako la mtumiaji na/au nywila yako imefichuliwa kwa yeyote yule, unakubali kutuarifu haraka iwezekanavyo kuhusu kufichuliwa huku ili OUP ichukue hatua mwafaka za kiusalama na ikupe jina jipya la mtumiaji na nywila mpya.


Utumiaji wa makala ya Tovuti

Unaruhusiwa ku:

1.  Tafuta, kuona, nyofoa, na kuonyesha sehemu fulani za makala ya Tovuti;

2.    hifadhi kielektroniki sehemu fulani za makala ya Tovuti;

3.    na/au kuchapisha nakala moja moja ya kila sehemu ya makala ya Tovuti unayoruhusiwa kuchapisha

Katika kila hali, kwa kuzingatia onyo za kipekee zinazopatikana katika kurasa mahususi za Tovuti. Hupaswi kuondoa wala kubadilisha ilani za hakimiliki au njia yoyote ya utambulisho au taarifa za kujiondoa hatiani kama zilivyo kwenye Tovuti; pia hupaswi kuchapisha nakala nyingi au kuwa na nakala nyingi za kielektroniki za sehemu za makala yaliyozuiwa kwa madhumuni yoyote isipokuwa kama inavyoruhusiwa kisheria au ilivyoidhinishwa na OUP; hupaswi kuonyesha au kusambaza sehemu yoyote ya data husika kwenye mtandao wowote wa kielektroniki, ikiwemo bali sio tu Intaneti na Mtandao wa Dunia Nzima; hupaswi kumruhusu yeyote afikie au atumie data hiyo; na/au hupaswi kutumia au kumruhusu yeyote atumie yote au sehemu yoyote ya data husika kwa shughuli zozote za kibiashara.

Ukijiandikisha kupokea vijarida au ukijiandikisha kupokea masasisho ya makala, unapaswa kutumia data uliyotumiwa kwa matumizi yasiyo ya kibiashara pekee. Hupaswi:

1.    kuondoa wala kubadilisha ilani za hakimiliki au njia yoyote ya utambulisho au taarifa za kujiondoa hatiani kama zilivyo kwenye data uliyotumiwa;

2.    kuchapisha nakala nyingi au kuwa na nakala nyingi za kielektroniki za sehemu za data hiyo kwa madhumuni yoyote isipokuwa kama inavyoruhusiwa kisheria au ilivyoidhinishwa na OUP;

3.    kuonyesha au kusambaza sehemu yoyote ya data husika kwenye mtandao wowote wa kielektroniki, ikiwemo bali sio tu Intaneti na Mtandao wa Dunia Nzima;

4.    kumruhusu yeyote afikie au atumie data hiyo; na/au

5.    kutumia yote au sehemu yoyote ya data husika kwa shughuli zozote za kibiashara.


Haki za Mali ya Kiakili

Sisi na/au watoa leseni wetu ndio wamiliki wa haki zote za mali ya kiakili kwenye Tovuti, na Tovuti na data iliyoko kwenye Tovuti zinalindwa na sheria za mali ya kiakili ulimwenguni ikiwa ni pamoja na sheria za hakimiliki na alama ya biashara. Kufuatia masharti ya ilani hii ya kisheria na mikataba mingine yoyote ya leseni kati yako na OUP, haki zote za aina hii zimehifadhiwa na hakuna data ambayo inapaswa kunakiliwa, kurekebishwa, kuchapishwa, kutangazwa au kusambazwa kwa namna yoyote bila idhini yetu ya awali iliyoandikwa. Oxford University Press, OUP, Oxford na/au majina yoyote yale ya bidhaa au huduma zozote zinazotolewa na Oxford University Press na yaliyotajwa kwenye Tovuti ni alama za biashara au alama za biashara zilizosajiliwa za Oxford University Press.

Licha ya yaliyotajwa hapo juu na inapotumika, hakimiliki katika kila mfano/picha iliyoko kwenye Tovuti inamilikiwa na mmiliki wa haki aliyetajwa kwenye dirisha la ‘Maelezo ya Picha’ la mfano/picha hiyo. Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna mfano/picha yoyote iliyoko kwenye Tovuti inayopaswa kunakiliwa, kurekebishwa, kuchapishwa au kutangazwa au kusambazwa kwa namna yoyote.


Viungo

Viungo vinavyokupeleka kwenye tovuti zingine vinatolewa na OUP na nia nzuri na kwa maelezo tu. OUP inajiondoa kwenye hatia inayotokana na data iliyoko kwenye tovuti yoyote iliyounganishwa kwa Tovuti hii.

Isitoshe, kiungo kinachokupeleka kwa tovuti isiyo ya OUP haimaanishi kuwa OUP inaidhinisha au inakubali wajibu utokanao na makala husika, au utumiaji, wa tovuti ya aina hii au bidhaa na/au huduma zinazotolewa kwenye tovuti ya aina hii. Ni jukumu lako kuchukua tahadhari ili uhakikishe kuwa unachochagua kukitumia hakina virusi, minyoo, trojani na vingine viharibifu.


Ufikiaji Huduma

Ingawa tunajizatiti kuhakikisha kuwa Tovuti hii inapatikana kwa kawaida kwa masaa 24 za siku, hatutawajibika ikiwa kwa sababu yoyote ile Tovuti hii haipatikani kwa wakati wowote au kwa kipindi chochote.

Ufikiaji Tovuti unaweza kusitishwa kwa mda mfupi na bila ilani ikiwa kuna hitilafu ya kimfumo, udumishaji au marekebisho au kwa sababu tusizoweza kudhibiti.


Malalamishi ya Ukiukaji wa Hakimiliki

OUP inaheshimu na kutilia maanani ulinzi wa haki za mali ya ubunifu. Ikiwa unaamini kuwa maudhui yoyote kwenye tovuti hii yanakiuka hakimiliki yako na ungependa yaondolewe, tafadhali tutumie ilani ya maandishi kwa njia ya barua pepe au posta ambayo inajumuisha:
(i) sahihi ya mkono au ya kielektroniki ya mmiliki wa hakimiliki au mtu aliyeidhinishwa kumwakilisha mmiliki wa hakimiliki.
(ii) Kitambulisho cha kazi ya hakimiliki inayodaiwa kukiukwa. Ikiwa kazi nyingi za hakimiliki kwenye tovuti moja zinaangaziwa na arifa moja, tupe orodha ya kazi kama hizo kwenye tovuti hiyo.
(iii) Kitambulisho cha nyenzo ambazo zinadaiwa kukiukwa (au kuhusika katika shughuli ya ukiukaji) ambazo zinatosha kuruhusu OUP kutambua na kupata eneo la nyenzo.
(iv) Anwani, nambari ya simu, na ikiwa ipo, anwani yako ya barua pepe ambayo tutatumia kuwasiliana nawe.
(v) Taarifa inayosema kwamba unaamini kwa nia njema kuwa matumizi ya nyenzo kwa njia iliyodaiwa haijaidhinishwa na mmiliki wa hakimiliki, wakala wake wala sheria.
(vi) Taarifa inayosema kwamba maelezo katika arifa ni sahihi na kwa mujibu wa adhabu ya kiapo cha uwongo, kuwa umeidhinishwa kumwakilisha mmiliki wa haki ya kipekee ambayo inadaiwa kukiukwa.

Tafadhali tuma ilani hii kwa wakala wa DMCA aliyeteuliwa:
Kupitia barua pepe: dmca@oup.com
Kupitia posta: Idara ya Sheria
Oxford University Press
Great Clarendon Street
Oxford
OX2 6DP
Uingereza


Makala kutoka kwa mtumizi

Sehemu fulani za Tovuti yetu huenda ziruhusu watumiaji wapakie makala yao wenyewe. Makala yaliyopakiwa na watumiaji hayawakilishi maoni ya OUP. Kwa kupakia makala kwenye Tovuti yetu, unakubali kufuata Maelekezo yetu. Unahakikisha kwamba makala ya aina hiyo yanafuata Maelekezo hayo na kuwa una haki zote zinazohitajika za data hizo na kuwa data hizo hazitakiuka wala kuvunja haki zozote za kibinafsi au za kimiliki za wahusika wowote wa kando tena data hizo hazina madhara yoyote (ikiwa ni pamoja na, bali sio tu, virusi vya kompyuta, bomu za kikompyuta, Trojani, minyoo, vitu vya kudhuru, data mbovu au programu nyingine zinazoweza kusababisha madhara au data yenye madhara).

OUP ina haki ya kuamua, bila kuhusisha uamuzi wa mwingine, kurekebisha, kuhariri au kufuta makala yoyote yaliyochapishwa na watumiaji, ambayo OUP inachukulia kuwa hayafuati Miongozo (kiungo) na/au yanamharibia mtu jina, yanakiuka sheria, yanatisha, yana lugha chafu au yanapingika kwa namna moja au nyingine. Licha ya yaliyotajwa hapo juu, OUP inajiondoa kwenye hatia inayotokana na makala yaliyopakiwa nawe au mtumiaji mwingine yeyote wa Tovuti. Pia, tuna haki ya kufichua utambulisho wako kwa watekelezaji sheria au kwa mhusika yeyote wa kando anayedai kwamba makala yoyote uliyoyachapisha au kupakia kwenye Tovuti yetu yanakiuka haki zao za mali ya kiakili, au haki yao ya faragha.


Haki ya OUP ya kutumia makala kutoka kwa mtumizi

Maudhui yoyote upakiayo kwenye Tovuti yetu yatachukuliwa kuwa yasiyo ya siri. Kwa vile OUP imekuruhusu utumie Tovuti hii kulingana na Ilani hii ya Kisheria (angalia Utumiaji wa maudhui ya Tovuti hapo juu), unaipa OUP leseni ya daima, ya ulimwenguni kote, isiyotengulika, isiyo na mirahaba, inayoweza kuhamishika, inayoweza kutumiwa na wengi ya kutumia, kuhariri, kuchanganua, kuchapisha, kuonyesha, kuwasiliana na umma kuyahusu na kuyatumia maradufu makala haya (au sehemu yao yoyote) katika lugha zote katika mfano wowote au chombo chochote kile iwe kipo au hakipo kwa sasa (na kutoa leseni hizi kwa wengine). Unajiondolea haki zozote za kimaadili kwa makala yoyote unayopakia kwenye Tovuti yetu (ikiwa ni pamoja na bali sio tu haki ya kutambuliwa kama mwandishi). Huenda tukupe heko kwa kazi yako lakini unakubali kwamba si lazima tufanye hivyo.


Makadirio

Tuna haki ya kufuatilia machapisho yote kwenye Tovuti kwa chochote kinachokiuka ilani hii ya kisheria na/au Maelekezo; kwa hivyo, machapisho mengine huenda yatumwe kwa makadirio kabla yachapishwe na, kutokana na hayo, huenda yachelewe kuonekana kwenye Tovuti.


Kusimamishwa na Kukomeshwa

Tutaamua, bila kuhusisha uamuzi wa mwengine, ikiwa Miongozo ama ilani hii ya kisheria imekiukwa [kiungo] kupitia utumiaji wako wa Tovuti. Wakati Miongozo ama ilani hii ya kisheria imekiukwa, tunaweza kuchukua hatua zifuatazo jinsi tunavyochukulia kuwa inafaa ikiwemo bali sio tu uzuiaji mtumiaji yeyote bila onyo wala majadiliano, anayekiuka Miongozo ama ilani hii ya kisheria, na tuondoe michango na machapisho yote ya awali.

Ukiukaji wa Miongozo ama ilani hii ya kisheria unaweza kusababisha uondolewaji wa papo hapo wa ufikiaji wako au haki yako ya kutumia Tovuti hii kwa mda mfupi au kabisa.


Hali ya Kimataifa ya Tovuti

Unatambua hali ya kimataifa ya Tovuti hii na kwa hivyo, unakubali kufuata sheria zote za ndani zinazotumika katika eneo lako unapotumia Tovuti.

Maelezo tunayoyachapisha kwenye Tovuti hii huenda yataje huduma na/au bidhaa zinazotolewa ambazo hazijatangazwa wala hazipo nchini mwako. Kutaja huku hakumaanishi kuwa tunanuia kutangaza huduma na/au bidhaa za aina hii nchini mwako.


Lugha

Ilani hii ya kisheria imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Ikiwa Ilani hii ya kisheria imetafsiriwa katika lugha nyingine yoyote, toleo lile la lugha ya Kiingreza ndilo litakalofuatwa.


Sheria Inayosimamia

Unakubali kwamba Ilani hii ya kisheria itasimamiwa kulingana na sheria za na mahakama zilizoko Uingereza na Wales. Licha ya yaliyotajwa hapo juu, hakuna chochote kilichopo kwenye ilani hii ya kisheria kitakachozuia OUP kuandikisha kesi katika mahakama yoyote kwa minajili ya kuchukua hatua dhidi ya ukiukaji wa haki zake za mali ya kiakili.


Taarifa kuhusu hadhi ya kiumiliki

Oxforddictionaries.com na tanzu zake huenda ijumuishe maneno yenye au yanayodaiwa kuwa na hadhi ya kiumiliki kama alama za biashara au nyingine. Kujumuishwa kwayo hakumaanishi kuwa yamepata kwa madhumuni ya kisheria, hadhi ya kawaida au hadhi isiyo ya kiumiliki wala hadhi yao ya kisheria haijaharibiwa vyovyote vile. Katika hali ambazo wafanyakazi wahariri wana uthibitisho kwamba neno lina hadhi ya umiliki hii huonyeshwa kwenye ingizo la neno hilo lakini huwa hawatoi maoni wala hawadokezi chochote kingine kuhusu hadhi yao ya kisheria kwa kufanya hivi.


Maoni na maelezo mengine yanayopatikana kwenye machapisho na maoni ya blogu ya OxfordWords hayawakilishi maoni au misimamo ya Oxford University Press.