Ufafanuzi msingi wa changa katika Kiswahili

: changa1changa2changa3

changa1

kitenzi elekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iza, ~iwa, ~wa

 • 1

  toa kitu au fedha ili kukusanya kwa makusudi fulani.

  ‘Changa fedha’

 • 2

  changanya karata.

 • 3

  chanja

Matamshi

changa

/t∫anga/

Ufafanuzi msingi wa changa katika Kiswahili

: changa1changa2changa3

changa2

kitenzi sielekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iza, ~iwa, ~wa

 • 1

  umwa viungoni au mishipani kama mgonjwa wa baridi yabisi.

Matamshi

changa

/t∫anga/

Ufafanuzi msingi wa changa katika Kiswahili

: changa1changa2changa3

changa3

kivumishi

 • 1

  -siokomaa k.v. tunda.

  ‘Embe changa’

 • 2

  -siopevuka.

  ‘Mimba changa’
  ‘Mtoto mchanga’

Matamshi

changa

/t∫anga/