Ufafanuzi msingi wa cheo katika Kiswahili

: cheo1cheo2

cheo1

nomino

 • 1

  kipimo cha nguo au kiatu.

  kiasi, kadiri, saizi, kilingo

 • 2

  daraja la mtu katika kazi.

  ‘Panda cheo’
  hadhi, kadiri, daraja, kiwango, ngazi

Ufafanuzi msingi wa cheo katika Kiswahili

: cheo1cheo2

cheo2

nomino

 • 1

  kifimbo cha chuma, shaba au pembe anachotumia mganga kupungia wagonjwa au kutafutia vitu vilivyopotea.

 • 2

  kibao cha kushonea ukili.

 • 3

  mti unaotumiwa kwa kufulia nazi.

  kifuo

Matamshi

cheo

/t∫ɛwɔ/