Ufafanuzi wa chombo katika Kiswahili

chombo

nominoPlural vyombo

 • 1

  kitu chochote cha kufanyia kazi.

  ‘Chombo cha seremala’
  zana, kifaa, ala

 • 2

  samani k.v. kochi, meza au kiti.

 • 3

  pambo la dhahabu la mwanamke k.v. pete, mkufu au bangili.

 • 4

  kifaa cha jikoni cha kupikia au kutilia chakula, maji, n.k. k.v. sahani, bakuli au chungu.

 • 5

  kitu kinachotumiwa kusafiria baharini k.v. jahazi, mashua, ngalawa, mtepe au meli.

 • 6

  muundo unaotekeleza kazi fulani na wenye madaraka fulani.

  ‘Chombo cha serikali’

Matamshi

chombo

/t∫ɔmbɔ/