Ufafanuzi msingi wa chuma katika Kiswahili

: chuma1chuma2

chuma1

nominoPlural vyuma

 • 1

  madini magumu yanayotumiwa kujengea na kuundia vitu.

  ‘Chuma cha pua’
  ‘Mabamba ya chuma’
  ‘Pao/Fito za chuma’
  ‘Chuma cha fuawe’
  hadidi

 • 2

  (ms) mtu mwenye nguvu; anayeweza kutegemewa.

  shujaa

 • 3

  silaha, hasa bastola au bunduki.

Matamshi

chuma

/t∫uma/

Ufafanuzi msingi wa chuma katika Kiswahili

: chuma1chuma2

chuma2

kitenzi elekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  tungua matunda au maua kutoka mtini.

 • 2

  fanya kazi, hasa biashara, na kupata faida ya mali au pesa nyingi.

Matamshi

chuma

/t∫uma/