Ufafanuzi wa fichuo katika Kiswahili

fichuo

nominoPlural mafichuo

 • 1

  zawadi au ada inayotolewa na bwana harusi kumpa bibi harusi anapomwona uso wake mara ya kwanza baada ya kumwoa.

 • 2

  ada anayopewa mwanamke anapovunja ungo au mwanamume anapotoka jandoni.

  tunzo

 • 3

  uvumbuzi

Matamshi

fichuo

/fit∫uwɔ/