Ufafanuzi wa geuka katika Kiswahili

geuka

kitenzi sielekezi~ia, ~ika

 • 1

  badilika kutoka hali moja na kuwa hali nyingine.

  ‘Hali ya hewa imegeuka leo’

 • 2

  badili uelekeo.

  ‘Nilipomwita aligeuka’

 • 3

  badili mawazo au msimamo.

Matamshi

geuka

/gɛwuka/