Ufafanuzi msingi wa hema katika Kiswahili

: hema1hema2

hema1

nominoPlural mahema

 • 1

  kibanda, agh. cha turubali, kinachotumiwa na wasafiri wanaokwenda kuishi mahali pasipo majumba k.v. porini au kwenye shamba.

  ‘Kita hema’
  ‘Piga hema’
  ‘Ng’oa hema’

Matamshi

hema

/hɛma/

Ufafanuzi msingi wa hema katika Kiswahili

: hema1hema2

hema2

kitenzi sielekezi~ea, ~eka, ~esha

 • 1

  tokwa na pumzi kwa nguvu k.v. baada ya kukimbia au kufanya kazi ya sulubu.

  bweta, tweta, haha, pwita

 • 2

  ‘Tunataka kuhema kidogo’
  tua, pumzika

Matamshi

hema

/hɛma/