Ufafanuzi wa kanyaga katika Kiswahili

kanyaga

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  weka mguu juu ya; gandamiza kwa mguu.

  vyoga, liwata

 • 2

  piga mtu barabara; twanga mtu au kitu.

  vyoga

 • 3

  fanya dhuluma; onea.

 • 4

  (ms) shinda katika jambo fulani.

  ‘Shule yetu imekanyaga shule ya jirani katika matokeo ya mtihani’

Matamshi

kanyaga

/ka3aga/