Ufafanuzi msingi wa kiasi katika Kiswahili

: kiasi1kiasi2kiasi3kiasi4

kiasi1

nominoPlural kiasi, Plural viasi

 • 1

  hali isiyozidi wala kupungua; hali ya wastani.

  ‘Kula kiasi’

 • 2

  kima maalumu cha kutosheleza.

  ‘Chota maji kiasi cha madebe mawili’
  kadiri, kifu, kipimo, kitembo, eneo, tani

 • 3

  thamani ya bei.

  ‘Nguo hii inauzwa kiasi gani?’

 • 4

  sehemu ya idadi ya kile kilichopo.

Asili

Kar

Matamshi

kiasi

/kijasi/

Ufafanuzi msingi wa kiasi katika Kiswahili

: kiasi1kiasi2kiasi3kiasi4

kiasi2

kivumishi

 • 1

  -a kutosha; -a wastani.

  ‘Amevuna chakula kiasi’

Matamshi

kiasi

/kijasi/

Ufafanuzi msingi wa kiasi katika Kiswahili

: kiasi1kiasi2kiasi3kiasi4

kiasi3

kielezi

 • 1

  kwa muda kidogo.

  ‘Tembea kiasi’

Matamshi

kiasi

/kijasi/

Ufafanuzi msingi wa kiasi katika Kiswahili

: kiasi1kiasi2kiasi3kiasi4

kiasi4

nominoPlural kiasi, Plural viasi

 • 1

  ganda la risasi.

Matamshi

kiasi

/kijasi/