Ufafanuzi wa mhuri katika Kiswahili

mhuri, muhuri

nominoPlural mihuri

  • 1

    kitu maalumu, agh. kilichotengenezwa kwa mpira, ubao au chuma, kinachopakwa wino na kugandamizwa kwenye kitu k.v. karatasi ili kuacha alama au maandishi yanayoonyesha mamlaka au uthibitisho.

  • 2

    alama au maandishi yanayoachwa na kitu hicho.

Matamshi

mhuri

/mhuri/