Ufafanuzi wa pengo katika Kiswahili

pengo

nominoPlural mapengo

 • 1

  nafasi iliyoachwa baada ya kung’oka jino.

 • 2

  nafasi iliyoachwa katika maandishi.

  ‘Jaza pengo kwa neno mwafaka kati ya yale uliyopewa’

 • 3

  nafasi inayokuwako baada ya mtu kuondoka au kitu kupungua.

  ‘Kifo chake kimeacha pengo kubwa’

Matamshi

pengo

/pɛngɔ/