Ufafanuzi msingi wa pima katika Kiswahili

: pima1pima2

pima1

nominoPlural pima

 • 1

  kipimo cha urefu kutoka kidole cha mkono mmoja hadi kidole cha mkono mwingine mikono inaponyooshwa kukingama mwili.

Matamshi

pima

/pima/

Ufafanuzi msingi wa pima katika Kiswahili

: pima1pima2

pima2

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  tafuta kiasi k.v. urefu, upana, uzito au wakati kwa kutumia chombo maalumu.

  ratili

 • 2

  fanya uchunguzi wa kitu.

  ‘Alikuja akanieleza maneno yake lakini nilipoyapima nikaona hayana maana’
  chungua, linga

 • 3

  enza, kadiria

Matamshi

pima

/pima/