Ufafanuzi msingi wa potea katika Kiswahili

: potea1potea2

potea1

kitenzi sielekezi~ana, ~lea, ~leana, ~leka, ~lewa, ~wa, ~za

 • 1

  kosekana na kutojulikana mahali kitu kilipo.

  ‘Kalamu yangu imepotea’
  hiliki

 • 2

  kosa kufuata njia ya sawa na kwenda mahali ambako hakukukusudiwa.

 • 3

  futika machoni.

  gea, toweka, ghibu

Matamshi

potea

/pɔtɛja/

Ufafanuzi msingi wa potea katika Kiswahili

: potea1potea2

potea2

kitenzi sielekezi~ana, ~lea, ~leana, ~leka, ~lewa, ~wa, ~za

 • 1

  kosa kufuata njia ya sawa au haki.

 • 2

  kosa kufuata mwongozo wa dini, maadili ya jamii au kanuni.

Matamshi

potea

/pɔtɛja/