Ufafanuzi msingi wa sakata katika Kiswahili

: sakata1sakata2sakata3

sakata1

kitenzi elekezi

 • 1

  tenda jambo kwa upesiupesi au uhodari.

  ‘Analisakata rumba’
  ‘Ameusakata wali wote’
  ‘Amemsakata ngumi’

Matamshi

sakata

/sakata/

Ufafanuzi msingi wa sakata katika Kiswahili

: sakata1sakata2sakata3

sakata2

nomino

 • 1

  msukumano na mvutano k.v. kwenye ghasia.

  ‘Kulikuwa na sakata kubwa’

Matamshi

sakata

/sakata/

Ufafanuzi msingi wa sakata katika Kiswahili

: sakata1sakata2sakata3

sakata3

nomino

 • 1

  tendo au tukio linalochukuliwa kijamii au kisheria kuwa ni kosa linalotendwa na maofisa k.v. serikalini au katika mashirika, na linaloleta aibu na kusababisha umma kulalamika, kuchukizwa na kukasirishwa k.v. wizi wa mali ya umma au ufisadi serikalini.

  kashfa

Matamshi

sakata

/sakata/