Ufafanuzi msingi wa tema katika Kiswahili

: tema1tema2

tema1

kitenzi elekezi~ea, ~eana, ~eka, ~ewa, ~wa, ~esha

 • 1

  kata sehemu ya kitu k.v. mwili au mti.

  ‘Alihukumiwa kwa kumtema mwenzako mkono’
  ‘Tema kuni’
  banja, vunja, pasua, chanja

Matamshi

tema

/tɛma/

Ufafanuzi msingi wa tema katika Kiswahili

: tema1tema2

tema2

kitenzi elekezi~ea, ~eana, ~eka, ~ewa, ~wa, ~esha

 • 1

  toa kitu kutoka mdomoni kwa makusudi na kukisukuma nje kwa ulimi.

  ‘Tema mate’

Matamshi

tema

/tɛma/