Ufafanuzi wa toa katika Kiswahili

toa

kitenzi elekezi~ana, ~ka, ~lea, ~lewa, ~za

 • 1

  ondoa kitu kilicho ndani ya kitu kingine, kundi au eneo maalumu.

  ‘Toa nje’
  ‘Toa uwanjani’

 • 2

  fanya kitu au jambo lisikike, lionekane au lifahamike.

  ‘Toa mfano’
  ‘Toa harufu’
  ‘Toa habari’
  ‘Toa sauti’

 • 3

  badilisha umilikaji wa kitu cha mtu mmoja ili kiwe cha mwingine.

  -pa

 • 4

  punguza idadi ya kitu katika hesabu; kinyume cha jumlisha.

Matamshi

toa

/tɔwa/