Ufafanuzi wa tumbukiza katika Kiswahili

tumbukiza

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~iwa, ~wa

 • 1

  ingiza kitu ndani ya kitu kingine k.v. ndani ya boksi, kisimani au shimoni.

 • 2

  tia ndani ya kitu k.v. mfukoni, majini, kapuni au shimoni.

 • 3

  ingiza mtu matatani.

  ‘Marafiki wa uongo wanaweza kukutumbukiza kwenye vitendo vya uhalifu’

Matamshi

tumbukiza

/tumbukiza/