Ufafanuzi wa wahi katika Kiswahili

wahi

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha

 • 1

  fika mahali au fanya jambo kwa wakati au kabla ya wakati; kuwa tayari.

  ‘Hakuwahi kufika mjini kwani gari lilimharibikia papa hapa’
  diriki, weza

 • 2

  tenda jambo mapema kabla halijaharibika.

 • 3

  tokea kufanya jambo.

  ‘Umewahi kugombea ubunge?’
  pata

Asili

Kar

Matamshi

wahi

/wahi/